KITABU; MIMI NI MSHINDI, Ahadi Yangu Na Nafsi Yangu.

Karibu rafiki upate kitabu MIMI NI MSHINDI, Ahadi yangu na nafsi yangu. Kitabu mimi ni mshindi kinakuwezesha wewe kuishi maisha ya ushindi, maisha ambayo yanakutofautisha wewe na wengine wengi ambao wanashindwa kufikia mafanikio makubwa.

Ukiangalia maisha ya washindi na maisha ya wale ambao wanashindwa yapo tofauti kabisa. Kuna namna ambavyo washindi wanachukulia mambo yao, wanavyotumia muda wao, wanavyotengeneza mahusiano yao na pia wanavyoshirikiana na wengine. Washindi wana njia tofauti za kuweka malengo ambayo wanayafikia na hivyo kuendelea kuwa washindi.

Kwa bahati mbaya sana maisha haya ya ushindi huwa hayafundishwi kwenye jamii zetu wala kwenye mfumo wetu wa elimu. Na hata wale wachache ambao wameweza kufikia ushindi, siyo wote ambao wana hamasa ya kuweza kuwashirikisha wengine mbinu zao. Kwa kukosa maarifa haya muhimu watu wengi wamekuwa wanafanya makosa ya wazi ambayo yanawazuia kufikia ushindi. Vitu kama uaminifu, matumizi mazuri ya muda, kuwa na shukrani ni vitu ambavyo kwa kawaida huwa hatuvipi uzito, lakini ndiyo vitu vyenye umuhimu mkubwa sana.

Kupitia kitabu hiki cha MIMI NI MSHINDI utajifunza mbinu zote za mafanikio na kazi yako inabaki kuzitumia kwenye maisha yako ili uweze kuwa na maisha ya ushindi.

Mambo gani mapya yaliyopo kwenye kitabu hiki?

Kama umekuwa ukisoma vitabu na makala ninazoandika, utakuwa unajua namna vitabu ninavyoandika vilivyo, sasa kitabu hiki kina haya ya ziada ambayo yatakupa maarifa zaidi na hamasa pia;

1. Kuna shuhuda za watu ambao wameshiriki mafunzo ya semina niliyotoa ya MIMI NI MSHINDI, wakielezea jinsi ambavyo mafunzo waliyopata yamebadili mtazamo wao kuhusu maisha yao na hatua wanazokwenda kuchukua. Kwa kusoma shuhuda hizi utaona ni jinsi gani inawezekana na kwako pia.

2. Kuna mifano halisi ya jinsi ambavyo mimi binafsi nimekuwa natumia mbinu hizi za ushindi unazokwenda kujifunza kwenye kitabu hiki na zikaniletea matokeo bora. Siishii tu kukuambia mbinu hii ni nzuri, bali nitakuonesha nimewezaje kuitumia mimi binafsi na kuweza kupata matokeo mazuri.

3. Kwenye kila sura kuna zoezi la wewe kufanya, hivyo unapomaliza kusoma sura moja ya kitabu hiki kuna zoezi utapewa la kufanya, zoezi hili linakuwezesha wewe kutumia kile ulichojifunza kwenye maisha yako. hutaishia kuwa na maarifa ya juu juu, badala yake utakuwa na namna ya kuyatumia maarifa hayo ili kupata matokeo bora.

4. Kitabu hiki kimeandikwa kwa nafsi ya kwanza, yaani kitabu kizima ni kama unajiambia wewe mwenyewe. Bada ya jina la kitabu kuwa WEWE NI MSHINDI, kwamba mimi nikuambie wewe, unajiambia wewe mwenyewe kwamba MIMI NI MSHINDI, na kitabu chote kipo hivyo, karibu kila kitu utakuwa unajiambia mwenyewe. Hii ina matokeo bora sana kisaikolojia kwa sababu inasisitiza umiliki wa kile unachojiambia.

5. Mwisho wa kitabu hiki kuna TAMKO KUU LA USHINDI, hapa unajipa tamko la ushindi ambalo lina misingi 20 utakayoisimamia. Kwa kujiambia tamko hili na kulirudia kila siku unajiweka kwenye nafasi nzuri ya kufanyia kazi yale uliyojifunza.

Kitabu hiki ni kizuri sana kwako kukisoma, kwani kitakufanya wewe ujishauri mwenyewe njia bora kwako kuchukua ili kufikia ushindi.

Kitabu hiki kinawafaa watu gani?

Kila kitabu kina watu wake, na hakuna kitabu kimoja ambacho kinamfaa kila mtu. Hivyo na kitabu hiki cha MIMI NI MSHINDI ni kwa wale ambao wanataka kuishi maisha ya ushindi, wale ambao wanataka kuwa na mafanikio makubwa kwenye maisha yao. Na mafanikio siyo kifedha pekee, bali kwenye kila eneo la maisha.

Wale ambao wamesharidhika na pale walipo, au wameshajiona wanajua kila wanachotaka kujua, kitabu hiki hakiwafai.

Pia wale ambao hawataki kuwa na maisha ya ushindi, wameshakubali kwamba wao ni wa chini na hakuna kinachoweza kuwatoa pale walipo kitabu hiki hakiwafai.

Lakini wale ambao wamekutana na changamoto kwenye maisha yao na wanaelekea kukata tamaa na kuona mambo hayawezekani, hiki ni kitabu kimoja wanachohitaji kukisoma haraka na kisha kurudi kwenye mapambano yao. Kwa sababu kupitia kitabu hiki utajifunza ni nini kimekufikisha hapo ulipo na namna gani ya kutoka hapo.

Mfumo wa kitabu na namna ya kukipata.

Kitabu hiki cha MIMI NI MSHINDI kipo kwenye mfumo wa softcopy (nakala tete) ambayo unaweza kusomea kwenye simu yako ambayo umekuwa unatumia kusomea makala za AMKA MTANZANIA. Pia unaweza kusomea kwenye tablet kama unayo na pia unaweza kusomea kwenye kompyuta kama unapendelea hivyo. Hii ni njia rahisi ya kujisomea vitabu na kuweza kutembea navyo popote unapokwenda.

Kitabu hiki kinatumwa kwa njia ya email na hivyo unaweza kukipata popote ulipo duniani bila hata ya kutoka hapo ulipo.

Gharama ya kitabu hiki ni tsh elfu kumi (10,000/=). Kupata kitabu hiki cha MIMI NI MSHINDI, tuma fedha tsh elfu 10 kwa MPESA 0755953887 au TIGO PESA/AIRTEL MONEY 0717396253 Majina kwenye namba hizo ni Amani Makirita. Ukishatuma fedha tuma ujumbe kwenye moja ya namba hizo yenye jina la kitabu MIMI NI MSHINDI pamoja na email yako na utatumiwa kitabu.

Karibu sana tuongeze maarifa kwa pamoja ili tuweze kuishi maisha ya ushindi yatakayotuwezesha kufikia mafanikio makubwa kwenye kila tunachofanya.

Kumbuka chochote unachotaka kwenye maisha yako kinaanza na wewe mwenyewe. Na ili uweze kuanzisha kile unachotaka unahitaji maarifa sahihi ya kufanya hivyo na sehemu mojawapo ya kupata maarifa haya ni kujisomea vitabu.

Nakutakia kila la kheri katika kutumia maarifa utakayoyapata kwenye kitabu hiki.

Rafiki na Kocha wako,

Makirita Amani,

makirita@kisimachamaarifa.co.tz

 

KITABU; BIASHARA NDANI YA AJIRA, JINSI YA KUANZISHA NA KUKUZA BIASHARA YAKO UKIWA BADO UMEAJIRIWA.

KITABU BIASHARA

BIASHARA NDANI YA AJIRA ni kitabu ambacho kinakupa mbinu za kuanzisha na kukuza biashara yako ukiwa bado umeajiriwa. Ni kitabu ambacho kila mwajiriwa anapaswa kukisoma kwa sababu kina maarifa muhimu ya kumwezesha mwajiriwa kujikomboa kiuchumi.

Wote ni mashahidi kwamba hali ya ajira kwa sasa imebadilika sana. Na kipato cha ajira kimekuwa hakitoshelezi. Na hata zile njia ambazo watu walikuwa wanatumia kujipatia kipato cha ziada kama posho, marupurupu na hata rushwa kwa sasa vimedhibitiwa kwa kiasi kikubwa.

Hivyo njia pekee kwa waajiriwa kuweza kujitengenezea uhuru wa kipato ni kuwa na vyanzo mbadala vya mapato. Kupitia kitabu hiki itajifunza mbinu za kuanzisha biashara na kuikuza. Pia itajifunza aina za biashara unazoweza kufanya ukiwa bado kwenye ajira. Utajifunza uwekezaji unaoweza kuanza kufanya ukiwa hapo kwenye ajira yako.

Kikubwa na muhimu zaidi utajifunza mifereji nane ya kipato unayotakiwa kujijengea ili kuweza kufikia uhuru wa kifedha. Utajifunza changamoto na hatari za kuepuka na pia kuweza kuilinda kazi yako pale unapofanya biashara.

Kitabu hiki ni mwongozo muhimu kwako kufikia uhuru wa kifedha kwa kuwa na biashara ya pembeni wakati umeajiriwa.

Soma kitabu hiki na yatumie yale ambayo umejifunza kwenye kitabu hiki katika kuboresha kazi yako na biashara yako pia. Na mwishowe utafikia uhuru wa maisha yako na mafanikio makubwa.

Nakutakia kila la kheri kwenye usomaji wa kitabu hiki, nina imani utajifunza mengi na utayatumia kwenye kazi yako, biashara yako na maisha yako kwa ujumla.

YALIYOMO kwenye kitabu hiki.

UTANGULIZI. 6

AJIRA NI SEHEMU NZURI YA KUANZIA BIASHARA. 7

HATARI YA KUCHOMA MELI MOTO. 11

UNA MUDA WA KUTOSHA. 15

CHANZO KIMOJA CHA KIPATO NI UTUMWA. 20

BIASHARA INAHITAJI MUDA KUKUA. 24

TENGENEZA MPANGO BORA KWAKO. 27

KUBALI KUPOTEZA. 31

BIASHARA UNAZOWEZA KUFANYA UKIWA BADO UMEAJIRIWA. 34

KIPAJI ULICHONACHO.. 34

UTAALAMU NA UZOEFU WAKO.. 37

BIASHARA ZA KAWAIDA. 39

BIASHARA YA MTANDAO.. 40

KILIMO CHA KIBIASHARA. 41

UWEKEZAJI UNAOWEZA KUFANYA UKIWA BADO UMEAJIRIWA. 43

UWEKEZAJI KWENYE MFUKO WA UMOJA. 43

UWEKEZAJI KWEYE SOKO LA HISA. 45

UWEKEZAJI KWENYE MALI 45

MAMBO YA KUZINGATIA UNAPOANZA BIASHARA UKIWA KWENYE AJIRA. 48

HATARI ZA KUEPUKA ILI BIASHARA YAKO IFANIKIWE. 54

KUWA NA MSHIRIKA. 58

USIFANYE KILA KITU PEKE YAKO. 61

FAIDA NYINGINE ZA KUENDELEA KUBAKI KWENYE AJIRA. 63

NIDHAMU.. 63

MTANDAO.. 64

RASILIMALI 65

MIFEREJI NANE YA KIPATO UNAYOHITAJI KUWA NAYO. 67

TENGENEZA MFUMO. 72

LINDA KAZI YAKO. 75

WAKATI SAHIHI WA KUONDOKA KWENYE AJIRA. 79

KITU MUHIMU KUFANYA MUDA WOTE. 85

ANZA SASA, NUNUA UHURU WAKO. 88
JINSI YA KUPATA KITABU HIKI;
Kitabu kinatumwa kama nakala tete yaani softcopy kwenye mfumo wa pdf. Kwa mfumo huu unaweza kusoma kitabu hiki kwenye simu yako kama ina uwezo wa kusoma vitabu na pia unaweza kusoma kwa kutumia kompyuta.
Kupata sura mbili za kitabu hiki na kuanza kukisoma sasa bonyeza maandishi haya na kupakua kitabu. Ili kupata kitabu kizima fuata utaratibu uliopo hapo chini.

Unatumiwa kitabu hiki kwa njia tatu, utachagua ile unayotaka wewe;
1. Kwa njia ya wasap, unaweza kutumiwa kwenye namba yako ya wasap na ukapakua kusoma.
2. Kwa njia ya telegram, pia unaweza kutumiwa kwenye namba yako ya telegram na ukapakua kusoma.
3. Kwa njia ya email, unaweza kutumiwa kitabu hiki moja kwa moja kwenye email yako.
Gharama ya kitabu hiki ni shilingi za Kitanzania elfu kumi tu (tsh 10,000/=). Ili kupata kitabu hiki tuma fedha kwenye namba zifuatazo;
1. Kama unatumia M- PESA tuma kwenda namba 0755 953 887 (jina AMANI MAKIRITA)
2. Kama unatumia TIGO PESA au AIRTEL MONEY tuma kwenda namba 0717 396 253 (jina AMANI MAKIRITA)
3. Kama upo nje ya Tanzania tuwasiliane kwa wasap 0717 396 253 au email na nitakupa utaratibu mzuri wa kulipia kulingana na ulipo.
Ukishatuma malipo ya kitabu, tuma ujumbe wa kawaida au wasap kwenda namba 0717 396 253 wenye jina la kitabu BIASHARA NDANI YA AJIRA na utatumiwa kitabu hiki kizuri.

Karibu sana rafiki yangu, ujipatie kitabu hiki ambacho kitakuwezesha kuanzisha na kukuza biashara yako ukiwa bado umeajiriwa.
Kama bado hujapata sura mbili za mwanzo za kitabu hiki zisome kwa kupakua kitabu hiki. Bonyeza maandishi haya na utapakua kitabu hiki na uanze kusoma.
TUPO PAMOJA,
Rafiki na Kocha wako,
Makirita Amani.

makirita@kisimachamaarifa.co.tz

KITABU; KURASA ZA MAISHA YA MAFANIKIO, TOLEO LA KWANZA 2016.

KURASA ZA MAISHA YA MAFANIKIO, TOLEO LA KWANZA 2016.

Habari njema kwa wana mafanikio wote, kitabu chako ambacho ndio mwongozo wa maisha ya mafanikio kwa mwaka huu 2016 tayari kimetoka. Kitabu hiki kinaitwa KURASA ZA MAISHA YA MAFANIKIO.

Hiki ni kitabu ambacho kinakupatia wewe maarifa sahihi ya kuishi maisha ya mafanikio, kwa vyovyote vile unavyoyapima mafanikio kwenye maisha yako. Safari ya mafanikio sio rahisi, kuna changamoto na vikwazo vingi, kuna kushindwa na kukatishwa tamaa na pia kuna kujisahau pale ambapo unakuwa umeshayapata mafanikio.

Ili kuweza kufikia mafanikio, kuvuka changamoto na kuwashinda wanaokukatisha tamaa, unahitaji mwongozo mzuri sana. Hapa ndipo unapokuja umuhimu wa kitabu unachoweza kukitumia kama mwongozo.

Kitabu KURASA ZA MAISHA YA MAFANIKIO kinagusa maeneo yote muhimu ya maisha yako na mafanikio pia. Kuanzia matumizi mazuri ya muda, jinsi ya kuzivuka changamoto unazokutana nazo kila siku, kujenga mahusiano bora na wanaokuzunguka na jinsi ya kuweka ubora zaidi kwenye kile unachokifanya.

Kitabu hiki kimeandaliwa kwa mfumo kwamba kila siku unasoma ukurasa mmoja wa kitabu hiki, na kila mwisho wa ukurasa kuna kauli chanya ambayo unajiambia. Kwa kufanya hivi kila siku unaanza na mtazamo chanya na kwa mtazamo huu chanya utaweza kufanikisha mengi. Pia kwa kusoma kurasa moja kwa siku unakuwa na kitu cha kufanyia kazi kila siku.

Ni watu gani wanahitaji sana kusoma kitabu hiki?

  1. Mtu yeyote ambaye anataka kufikia mafanikio makubwa kwenye maisha yake.
  2. Wafanyakazi ambao wamekuwepo kwenye ajira muda mrefu lakini hawaoni wakisonga mbele, kila mwaka wako pale pale.
  3. Wafanyabiashara ambao wanataka kukuza biashara zao zaidi ya zilipo sasa.
  4. Mtu yeyote ambaye ameshakata tamaa na maisha na kuona hakuna kitu kizuri kinachoweza kutokea kwenye maisha yake.
  5. Mtu yeyote anayependa kujifunza na kuhamasika kila siku, ili kuweza kuweka juhudi zaidi kwenye maisha yake.

Kitabu hiki ni kuzuri sana kwa kila mtu, hivyo usikose kukisoma.

Kwa nini ni muhimu sana wewe kukisoma kitabu hiki?

Ni muhimu wewe hapo upate kitabu hiki na ukisome, kwa sababu zifuatazo;

  1. Unahitaji kujifunza kila siku na kuhamasika. Kitabu hiki kina kurasa zinazolingana na siku za mwaka hivyo kila siku utakuwa na kitu cha kujifunza.
  2. Unahitaji mbinu bora za kutatua changamoto ulizonazo, kutatua changamoto kwa mbinu zile zile ni kupoteza muda wako. Kitabu hiki kina mbinu nyingi nzuri.
  3. Unahitaji kujenga mahusiano bora kwako mwenyewe na wale wanaokuzunguka, utajifunza zaidi kwenye kitabu hiki.
  4. Unahitaji kubadili mtazamo wako kuhusu fedha, kama bado unapata changamoto za kifedha. Kitabu hiki kinakupa mbinu za kuongeza kipato, kukilinda na kisha kuweka akiba na kuwekeza zaidi.
  5. Unahitaji kuwa chanya kila siku, kwenye dunia iliyojaa watu hasi. Kwa idadi ya watu hasi wanaokuzunguka, upo kwenye hatari ya wewe kuwa hasi pia. Kwa kusoma kitabu hiki kila siku utaendelea kuwa chanya kila siku.

Hiki ni kitabu ambacho hupaswi kabisa kukikosa kama kweli umedhamiria kuishi maisha bora kwako na yatakayokuletea mafanikio makubwa bila ya kujali unafanya nini.

Jinsi ya kukipata kitabu; KURASA ZA MAISHA YA MAFANIKIO.

Kitabu hiki kipo kwenye mfumo wa kielektroniki yaani softcopy (pdf). Kwa mfumo huu, kitabu hiki unaweza kukisomea kwenye simu yako ya mkononi, kwenye tablet au kwenye kompyuta. Kwa njia hii ni rahisi sana kuwa na kitabu hiki popote pale ulipo, hata kama umesafiri, ukitaka kukisoma ni kufungua tu kwenye simu yako. na hii ni muhimu kwa sababu hiki ni kitabu cha kusoma kila siku kwa mwaka mzima.

Kitabu hiki kinatumwa kwa njia ya email, hivyo popote pale ulipo duniani, unaweza kutumiwa kitabu hiki. Huhitaji kwenda popote kukifuata, kinakufuata hapo ulipo wewe.

Gharama ya kitabu hiki ni tsh elfu kumi (10,000/=).

Kupata kitabu hiki tuma fedha kwa njia ya mtandao wa simu kama ifuatavyo;

M-PESA; 0755 953 887 (JINA AMANI MAKIRITA)

TIGO PESA; 0717 396 253 (JINA AMANI MAKIRITA)

AIRTEL MONEY; Tuma moja kwa moja kwenda namba ya tigo pesa 0717 396 253

Ukishatuma fedha tuma ujumbe kwenye moja ya namba hizo hapo juu, ujumbe uwe na email yako pamoja na jina la kitabu kisha utatumiwa kitabu.

Karibu sana upate kitabu hiki cha KURASA ZA MAISHA YA MAFANIKIO, kipate mapema ili ujihakikishie kuwa na maisha bora kwa mwaka huu 2016.

Nakutakia kila la kheri katika safari yako ya mafanikio, kumbuka hakuna wa kukuzuia bali wewe mwenyewe. Usikubali kujizuia.

Rafiki na Kocha wako,

Makirita Amani,

makirita@kisimachamaarifa.co.tz

KITABU; JINSI YA KUFAIDIKA NA MABADILIKO YANAYOTOKEA KWENYE MAISHA.

JINSI YA KUFAIDIKA NA MABADILIKO YANAYOTOKEA KWENYE MAISHA.

Kama kuna kitu kimoja ambacho tuna uhakika nacho hapa duniani ni kwamba dunia inabadilika kila siku. Ukiangalia historia ya dunia tulikotoka na tulipo sasa kumetokea mabadiliko makubwa sana. Zilianza zama za mawe, zikaja zama za chuma, yakaja mapinduzi ya viwanda na hata sasa tupo kwenye mapinduzi ya kiteknolojia.

Jambo moja la kushangaza ni kwamba pamoja na mabadiliko haya kuwa wazi bado watu wengi ni wagumu sana kubadilika. Watu hawapendi mabadiliko, wanapenda kufanya kile walichozoea kufanya na wanataka maisha yaendelee vile yalivyokuwa jana na leo. Kitu ambacho ni ndoto isiyowezekana.
Katika zama zote ambazo dunia imepita, kuna watu ambao waliweza kubadilika haraka na kupata faida ya mabadiliko, wengine walilazimishwa kubadilika na hivyo kuburuzwa na kuna ambao waliachwa na mabadiliko na hivyo kupotea. Waliofaidika na mabadiliko ni wale waliokuwa tayari kubadilika, walioburuzwa na mabadiliko ni wale ambao walikuwa hawajui kama kuna mabadiliko ila wanakwenda tu na hali ilivyo. Walioachwa na mabadiliko ni wale ambao hata baada ya kuona mabadiliko wao waligoma kubadilika, waliendelea kung’ang’ania kile walichozoea na hatimaye kuachwa nyuma na kupotea.

Mabadiliko ni jambo muhimu sana lakini watu wengi hawajalipa msisitizo kwenye maisha na hii inapelekea wengi kuachwa nyuma na mabadiliko haya.
Ni kutokana na umuhimu wa jambo hili nimekuandalia kitabu kinachoitwa JINSI YA KUFAIDIKA NA MABADILIKO YANAYOTOKEA KWENYE MAISHA.

Katika kitabu hiki utajifunza mambo yafuatayo;
1. Historia fupi ya mabadiliko kwenye maisha ya mwanadamu hapa duniani na kwa nini mabadiliko yataendelea kutokea.
2. Mabadiliko makubwa yanayotokea kwenye elimu, kazi na hata biashara.
3. Makundi ya aina tatu ya watu ambao wanazalishwa na mabadiliko, kundi linalonufaika na mengine yanayopoteza.
4. Mambo kumi muhimu sana ya kufanya ili na wewe uingie kwenye kundi ambalo linanufaika sana na mabadiliko ambayo yanaendelea kutokea
5. Mabadiliko makubwa yanayokuja kwenye mfumo wa elimu, mfumo wa ajira na hata biashara na ujasiriamali.
Kitabu hiki kitakuandaa wewe na kukupa mbinu za kuweza kuboresha maisha yako zaidi na kufanikiwa licha ya mabadiliko yanayoendelea.
Kitabu hiki ni muhimu sana kwa makundi yafuatayo;
1. Wanafunzi wa vyuo vikuu ambao wanasoma ila hawana uhakika wa kupata ajira. Kitawawezesha kujiandaa mapema ili kujua njia watakayochukua na hivyo kutopoteza muda wakisubiri ajira ambazo hazipo.
2. Wafanyakazi ambao wamekuwa kwenye kazi kwa muda mrefu lakini hawaoni manufaa ya kazi zao kwenye maisha yao.
3. Wafanyabiashara ambao wamefanya biashara kwa muda mrefu ila wako pale pale miaka nenda miaka rudi.
4. Wafanyakazi ambao wamestaafu kazi, wamefukuzwa kazi, wamepunguzwa kazi au wameamua kuacha kazi wenyewe.
5. Watu ambao umri wao umekwenda kiasi na wanaamini kwamba mambo waliyokuwa wanafanya zamani ni bora kuliko yanayofanyika sasa, na wanaendelea kuyafanya licha ya kushindwa kupata majibu makubwa.
6. Mtu yeyote ambaye anataka kuboresha maisha yake zaidi, kwa kujua mambo yanayoendelea na ni yapi yanakuja kwa siku za mbeleni.
Ni muhimu sana wewe kupata na kusoma kitabu hiki, kitaleta mabadiliko makubwa sana kwenye maisha yako kama utakuwa tayari kufanyia kazi yale ambayo utajifunza.
 

JINSI YA KUPATA KITABUJINSI YA KUFAIDIKA NA MABADILIKO YANAYOTOKEA KWENYE MAISHA.
Kitabu hiki kipo kwenye mfumo wa soft copy yaani pdf na unaweza kukisoma kwenye simu yako kama ni smartphone, unaweza kukisoma kwenye tablet na pia unaweza kukisoma kwenye kompyuta. Kurasa zake zinasomeka vizuri kwenye vifaa hivyo vya aina tatu tofauti.
Gharama ya kitabu hiki ni tsh elfu tano(5,000/=), gharama hii ndogo sio kwa sababu kina mambo madogo ila ni kwa sababu kitabu hiki ni muhimu sana na kila mtu ni muhimu akisome ndiyo maana nimefanya ndogo ili isiwe kikwazo cha watu kushindwa kukisoma.
Kupata kitabu hiki tuma fedha kwa njia ya mtandao wa simu kama ifuatavyo;

M-PESA; 0755 953 887 (JINA AMANI MAKIRITA)

TIGO PESA; 0717 396 253 (JINA AMANI MAKIRITA)

AIRTEL MONEY; Tuma moja kwa moja kwenda namba ya tigo pesa 0717 396 253

Ukishatuma fedha tuma ujumbe kwenye moja ya namba hizo hapo juu, ujumbe uwe na email yako pamoja na jina la kitabu kisha utatumiwa kitabu.
Mambo sasa hivi yanakwenda kidigitali zaidi na huna haja ya kubeba mizigo mingi, kwa kuwa na simu yako tu unaweza kuendelea kujifunza mambo mengi sana.
Karibu sana upate kitabu hiki mapema, kwa sababu jinsi unavyozidi kuchelewa kukipata, mabadiliko yanaendelea kutokea na yanakuacha nyuma. Jinsi utakavyoweza kuchukua hatua haraka ndivyo unavyoweza kuiokoa na kuimarisha kazi yako au biashara yako. Chukua hatua haraka kwa kusoma kitabu hiki leo.

Nunua vitabu ili kuongeza maarifa na uweze kufanya maamuzi sahihi.

Karibu sana,

TUPO PAMOJA,

Rafiki na Kocha wako,

Makirita Amani,

makirita@kisimachamaarifa.co.tz

KITABU; JINSI YA KUTENGENEZA FEDHA KWENYE MTANDAO KWA KUTUMIA BLOG.

JINSI YA KUTENGENEZA FEDHA KWENYE MTANDAO KWA KUTUMIA BLOG.

Tunaishi kwenye ulimwengu wa zama za taarifa. Katika ulimwengu huu wale wenye taarifa sahihi ndio wanaonufaika kuliko wale ambao hawana taarifa sahihi. Pia katika ulimwengu huu taarifa watu wengi wameweza kunufaika kwa kuuza taarifa ambazo wanazo na wengine wanazihitaji.

Je na wewe upo tayari kunufaika na taarifa ulizonazo, ambazo zinaweza kuwanufaisha wengine? Kama jibu ni ndiyo basi kuna njia moja nzuri kwako kuweza kuuza taarifa zako kwa wengine. Na njia hii ni kumiliki blog ambayo unaweza kuiendesha kibiashara.

Unaweza kujifunza jinsi ya kuuza taarifa zako kupitia kitabu nilichoandika kinachoitwa JINSI YA KUTENGENEZA PESA KWENYE MTANDAO KWA KUTUMIA BLOG. Kitabu hiki kimejaa mbinu muhimu za kutengeneza fedha ambazo zinafanya kazi kwenye mazingira yetu ya Kitanzania na ndio huwa nazitumia kila siku.

Katika kitabu hiki utajifunza jinsi ya kutengeneza blog hata kama hujui na hujawahi kujifunza kutengeneza blog. Kitabu hiki kina maelekezo rahisi ya Kiswahili pamoja na picha ambazo zinakuwezesha kutengeneza blog yako mwenyewe.

Baada ya kutengeneza blog yako unajifunza jinsi ya kuikuza blog hiyo kwa kuandika makala nzuri na ambazo zinawasaidia watu kutatua changamoto zao. Pia utajifunza mbinu za kuweza kuwafikia wasomaji wengi zaidi ili blog yako iweze kukua.

Mwisho utajifunza jinsi ya kuibadili blog yako na kuwa biahsara ambayo inakuingizia kipato. Utajifunza huduma mbalimbali unazoweza kuuza kupitia blog yako na pia utajifunza mbinu bora za uuzaji kupitia mtandao wa intaneti.

Yaliyomo kwenye kitabu.
Kitabu hiki kina mafunzo yafuatayo;
1. Utambulisho wa blog na aina mbalimbali za blog.
2. Jinsi ya kutengeneza blog
3. Njia mbalimbali za kutengeneza fedha kupitia blog.
4. Kuweka misingi ya blog yako na kuchagua mtindo wako.
5. Uandishi wa makala zenye mvuto.
6. Kujenga hadhira na kuvutia wasomaji wengi zaidi(email list).
7. Kuunganisha blog na mitandao mingine ya kijamii ili kupata wasomaji wengi zaidi.
8. Kuchagua njia ya kuingiza fedha kutumia blog.
9. Uandishi wa makala za kuuzia bidhaa au huduma na siri iliyoko nyuma ya utafutaji wa masoko.
10. Kutengeneza fedha kusiko na kikomo kupitia blog yako.
11. Kutofautisha blog yako na blog nyingine na jinsi ya kuendelea kuikuza zaidi.
Masomo hayo yameelezewa kwa lugha rahisi na wakati mwingine kwa kutumia picha ili kuweza kukurahisishia wewe kuelewa.

Pata kitabu hiki mara moja ili uweze kutengeneza misingi yako ya kuweza KUTENGENEZA KIPATO KISICHO NA KIKOMO KWENYE MTANDAO KWA KUTUMIA BLOG. Uzuri wa kutengeneza pesa kwenye mtandao ni kwamba hakuna kikomo na unaweza kufanya kazi popote ulipo. Kikomo cha kiwango cha fedha unachoweza kutengeneza unaweka mwenyewe, ukiwa na juhudi na maarifa kipato kinakuwa kikubwa. Unaweza kufanyia kazi zako ofisini, nyumbani au sehemu yoyote unayoona ni nzuri kwako.
Kupitia kitabu hiki unapata nafasi kubwa ya kuyaboresha maisha yako.
Karibu sana upate kitabu hiki ambacho kitaboresha maisha yako kwa kiasi kikubwa sana.
Jinsi ya kupata kitabu hiki;

Kitabu hiki kipo kwenye mfumo wa soft copy yaani pdf. Huu ni mfumo wa nakala tete ya kitabu ambapo unaweza kukisoma kitabu hiki kwenye simu yako kama unatumia smartphone, unaweza kusomea kwenye tablet na pia unaweza kusomea kwenye kompyuta yako.

Kitabu hiki kinatumwa kwa njia ya email hivyo kinaweza kukufikia popote ulipo duniani dakika chache baada ya kukilipia.

Gharama ya kitabu hiki ni tsh elfu kumi (10,000/=).

Kupata kitabu hiki tuma fedha kwa njia ya mtandao wa simu kama ifuatavyo;

M-PESA; 0755 953 887 (JINA AMANI MAKIRITA)

TIGO PESA; 0717 396 253 (JINA AMANI MAKIRITA)

AIRTEL MONEY; Tuma moja kwa moja kwenda namba ya tigo pesa 0717 396 253

Ukishatuma fedha tuma ujumbe kwenye moja ya namba hizo hapo juu, ujumbe uwe na email yako pamoja na jina la kitabu kisha utatumiwa kitabu.

Nunua vitabu ili kuongeza maarifa na uweze kufanya maamuzi sahihi.

Karibu sana,

TUPO PAMOJA,

Rafiki na Kocha wako,

Makirita Amani,

makirita@kisimachamaarifa.co.tz

KITABU; KWA NINI MPAKA SASA WEWE NI SIO TAJIRI.

KWA NINI MPAKA SASA WEWE SIYO TAJIRI

Madhumuni ya kuandika kitabu hiki ni kuwasaidia wale wote wenye

malengo ya kufanikiwa kwenye maisha yao na kuwa matajiri. Kwa

bahati mbaya sana kwenye mfumo wa elimu hakuna sehemu ambapo tunafundishwa somo linalohusiana na kutengeneza utajiri.

Wachache wanaojua siri za kupata utajiri wamekuwa wakinufaika nazo na wengi ambao hawajui siri hizi wamekuwa wakiteseka kila siku kuendesha maisha yao.

Kupitia kitabu hiki utajifunza sababu ishirini na tano ambazo zinakuzuia wewe kuwa tajiri. Na kwa kila sababu utakayojifunza utapewa hatua za kuchukua ili kuweza kuondokana na sababu hiyo na kufikia utajiri.

Kitabu hiki kinamfaa mtu yeyote ambaye ana malengo makubwa ya kufanikiwa kwenye maisha yake na kuwa tajiri. Kwa kusoma na kutumia mafunzo haya kutamsaidia yeyote mwenye lengo la kuwa tajiri kufikia lengo lake.

Yaliyomo kwenye kitabu hiki;

Utangulizi.

Wewe ni masikini.

Sababu ya kwanza; Hujaamua kuwa tajiri.

Sababu ya pili; Huna mpango na maisha yako.

Sababu ya tatu; Unafanya kile ambacho kila mtu anafanya.

Sababu ya nne; Hufurahii unachofanya.

Sababu ya tano; Unafikiri kuna mtu atakuja kukutoa hapo ulipo.

Sababu ya sita; Unafikiri huna bahati.

Sababu ya saba; Unafikiri kuna njia ya mkato ya kupata utajiri.

Sababu ya nane; Una mtizamo hasi kuhusu biashara na maisha.

Sababu ya tisa; Mfumo wa elimu umekuharibu.

Sababu ya kumi; Unataka kufanya kila kitu.

Sababu ya kumi na moja; Una matumizi mabovu ya hela.

Sababu ya kumi na mbili; Unamfanyia mtu mwingine kazi.

Sababu ya kumi na tatu; Umezungukwa na watu ambao wana mawazo ya kimasikini.

Sababu ya kumi na nne; Hujali muda.

Sababu ya kumi na tano; Hujawahi kuchukua hatua.

Sababu ya kumi na sita; Huna washauri wazuri.

Sababu ya kumi na saba; Umetawaliwa na woga.

Sababu ya kumi na nane; Unalalamika sana.

Sababu ya kumi na tisa; Unafanya kila kitu mwenyewe.

Sababu ya ishirini; Huwekezi kwenye maendeleo yako binafsi.

Sababu ya ishirini na moja; Hujali afya yako.

Sababu ya ishirini na mbili; Unakata tama mapema.

Sababu ya ishirini na tatu; Hujatoa kafara.

Sababu ya ishirini na nne; Unafikiri muda bado.

Sababu ya ishirini na tano; Huna nidhamu.

 

Jinsi ya kupata kitabu hiki;

Kitabu hiki kipo kwenye mfumo wa soft copy yaani pdf. Huu ni mfumo wa nakala tete ya kitabu ambapo unaweza kukisoma kitabu hiki kwenye simu yako kama unatumia smartphone, unaweza kusomea kwenye tablet na pia unaweza kusomea kwenye kompyuta yako.

Kitabu hiki kinatumwa kwa njia ya email hivyo kinaweza kukufikia popote ulipo duniani dakika chache baada ya kukilipia.

Gharama ya kitabu hiki ni tsh elfu tano (5,000/=).

Kupata kitabu hiki tuma fedha kwa njia ya mtandao wa simu kama ifuatavyo;

M-PESA; 0755 953 887 (JINA AMANI MAKIRITA)

TIGO PESA; 0717 396 253 (JINA AMANI MAKIRITA)

AIRTEL MONEY; Tuma moja kwa moja kwenda namba ya tigo pesa 0717 396 253

Ukishatuma fedha tuma ujumbe kwenye moja ya namba hizo hapo juu, ujumbe uwe na email yako pamoja na jina la kitabu kisha utatumiwa kitabu.

Nunua vitabu ili kuongeza maarifa na uweze kufanya maamuzi sahihi.

Karibu sana,

TUPO PAMOJA,

Rafiki na Kocha wako,

Makirita Amani,

makirita@kisimachamaarifa.co.tz